Acts 18:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Apolo alianza kunena kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikia, walimwalika kwao na kumweleza njia ya Mungu kwa ufasaha zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Apolo alianza kuzungumza kwa ujasiri katika sinagogi. Prisila na Akila walipomsikia akizungumza, walimchukua wakaenda naye nyumbani mwao kisha wakamsaidia kuielewa njia ya Mungu vizuri zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo Njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Apolo alianza kunena kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi, Lakini Prisila na Akila walipomsikia walimchukua kando na kumweleza njia ya Mungu kwa ufasaha zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Apolo alianza kunena kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikia, walimchukua kando na kumweleza njia ya Mwenyezi Mungu kwa ufasaha zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Priskila na Akila walipomsikia wakampeleka kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo alipoanza kutangaza nyumbani mwa kuombea waziwazi, Puriskila na Akila wakamsikia nao, wakampokea, wakamfunulia vema njia ya Mungu, aijue kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye akaanza kusema pasipo woga katika nyumba ya kuabudia. Prisila na Akila walipomusikia, wakaenda naye kwao na kumufasiria Njia ya Mungu kwa ukweli zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaanza kunena bila khofu katika sunagogi: hatta Akula na Priskilla walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.