Acts 18:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, akakaa na kufanya kazi pamoja nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walikuwa watengenezaji wa mahema, kama alivyokuwa Paulo, hivyo alikaa na kufanya kazi pamoja nao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama alivyokuwa yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, akakaa na kufanya kazi pamoja nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, akakaa na kufanya kazi pamoja nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa sababu kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi; maana walikuwa mafundi wa kushona mahema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akakaa na kutumika pamoja nao, kwa maana wote walikuwa wafundi wa kutengeneza hema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akafika kwao; na kwa kuwa kazi yake na kazi yao ni moja, akakaa kwao, akafanya kazi yake, kwa maana walikuwa mafundi wa kufanyiza khema.