Acts 18:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto, ambaye nyumba yake ilikuwa karibu na lile sunagogi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akaondoka kwenye sinagogi, akaenda nyumbani mwa Tito Yusto, aliyekuwa mcha Mungu; nyumba yake ilikuwa karibu na sinagogi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Tito Yusto, mcha Mungu, ambaye nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sinagogi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo aliondoka katika sinagogi na kuhamia nyumbani kwa Tito Yusto, mtu aliyekuwa anamwabudu Mungu wa Kweli, nyumba yake ilikuwa jirani na sinagogi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwa karibu na lile sunagogi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto, ambaye nyumba yake ilikuwa karibu na lile sunagogi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akaondoka mle kwenye sinagogi, akaenda nyumbani kwa mtu mmoja jina lake Tito Yusto, aliyekuwa mcha Mungu. Nyumba yake ilikuwa jirani na Sinagogi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akaondoka mle kwenye sinagogi, akaenda nyumbani kwa mtu mmoja jina lake Tito Yusto, aliyekuwa mcha Mungu. Nyumba yake ilikuwa karibu na sinagogi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Tito Yusto, mcha Mungu, ambaye nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sinagogi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto, ambaye nyumba yake ilikuwa karibu na lile sunagogi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaondoka mle, akaingia nyumbani mwa mtu mwenye kumcha Mungu, jina lake Tiro Yusto, ambaye nyumba yake ilikuwa imepakana na nyumba ya kuombea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Tito Yusto, mcha Mungu, ambaye nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sinagogi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Paulo akaondoka pale, akaenda kukaa katika nyumba ya mutu mumoja aliyeitwa Tito Yusto, aliyekuwa mwenye kuogopa Mungu. Nyumba ya mutu huyu ilikuwa karibu sana na nyumba ya kuabudia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Yusto, mcha Mungu, ambae nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sunagogi.