Acts 18:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Krispo, mkuu wa hilo sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana, yeye pamoja na watu wote wa nyumbani mwake. Nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo pia wakaamini na kubatizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Krispo aliyekuwa kiongozi wa sinagogi lile, pamoja na watu wote waliokuwa wanaishi nyumbani mwake walimwamini Bwana Yesu. Watu wengi katika mji wa Korintho walimsikiliza Paulo, wakaamini na wakabatizwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Krispo, mkuu wa sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Krispo, mkuu wa hilo sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana pamoja na wote wa nyumbani mwake, nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo wakaamini na kubatizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana Isa, yeye pamoja na watu wote wa nyumbani mwake. Nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo pia wakaamini na kubatizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Krispo, mkuu wa hilo sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Krispo aliyekuwa mkubwa wa nyumba ya kuombea alimtegemea Bwana pamoja na waliokuwamo nyumbani mwake wote. Hata wenyeji wa Korinto wengi walipovisikia wakamtegemea, wakabatizwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na Krispo, mukubwa wa nyumba ya kuabudia, akamwamini Bwana pamoja na watu wote wa nyumba yake. Nao Wakorinto wengi waliomusikiliza Paulo wakaamini na kubatizwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Krispo, mkuu wa sunagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi wakasikia, wakaamini, wakabatizwa.