Acts 19:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya walisafiri huko na huko wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: “Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya Wayahudi waliotangatanga wakitoa pepo wachafu wakajaribu kutumia jina la Bwana Isa kwa wale wenye pepo, wakisema, “Kwa jina la Isa, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia baadhi ya Wayahudi walikuwa wanasafiri huku na huko wakiwatoa pepo wabaya kwa watu. Wana saba wa Skewa, mmoja wa viongozi wa makuhani, walikuwa wakifanya hili. Wayahudi hawa walijaribu kutumia jina la Bwana kuyatoa mapepo kwa watu. Wote walikuwa wanasema, “Katika jina la Bwana Yesu anayezungumzwa na Paulo ninakuamuru utoke!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya, walisafiri huko na huko, wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: “Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya walisafiri huko na huko wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: “Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga huku na huko wakitoa pepo wachafu wakajaribu kutumia jina la Bwana Yesu juu ya wale wenye pepo wakisema, “Kwa jina la Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga huku na huko wakitoa pepo wachafu, wakajaribu kutumia jina la Bwana Isa kwa wale wenye pepo, wakisema, “Kwa jina la Isa, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya walisafiri huko na huko wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: “Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na wapunga pepo wa Kiyuda waliozunguka hapo, wakajaribu kuwatajia waliopagawa na pepo wabaya Jina la Bwana Yesu, wakisema: Nawaapiza kwa nguvu ya Yesu, Paulo anayemtangaza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kulikuwa Wayuda wamoja waliotangatanga huku na huko kwa kufukuza pepo. Watu wale wakajaribu vilevile kutaja jina la Bwana Yesu, wakiwaambia vilevile pepo: “Ninawaamuru muondoke kwa jina la Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni waganga wa pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Twawaapizeni kwa Yesu, yule anaekhubiriwa na Paolo.