Acts 19:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha mtu aliyekuwa na pepo ndani yake akawarukia. Alikuwa na nguvu kuliko wote. Akawapiga, akawachania nguo za na kuwavua, nao wakakimbia kutoka katika nyumba ile wakiwa uchi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile wakiwa uchi na kujeruhiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha yule mtu mwenye pepo mbaya akawarukia, akawakamata wawili, akawafanyizia vibaya kwa nguvu zake, mpaka wakakimbia mle nyumbani wenye uchi na wenye madonda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na yule mutu aliyekuwa na pepo ndani yake akawarukia, akawashinda wote nguvu na kuwatendea vibaya hata wakakimbia toka nyumba yake wakiwa uchi na wakijaa vidonda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia, akawaweza, akawashinda, hatta wakatoka mbio katika nyumba ile uchi na wamejeruhi.