Acts 19:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Nao wakamjibu, “La! Hata hatujasikia kwamba kuna Roho Mtakatifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akawauliza, “Je, mlipokea Roho wa Mungu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho wa Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akawauliza, “Mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wafuasi hao wakamwambia, “Hatujawahi hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Nao wakamjibu, “La! Hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatujasikia.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Nao wakamjibu, “La! Hata hatujasikia kwamba kuna Roho Mtakatifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akawauliza, “Je, mlipokea Roho wa Mwenyezi Mungu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho wa Mwenyezi Mungu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Nao wakamjibu, “La! Hata hatujasikia kwamba kuna Roho Mtakatifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawauliza: Mmepewa Roho takatifu mlipoanza kumtegemea Bwana? Nao wakamjibu: Hapana, hatujasikia, kama iko Roho takatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akawauliza: “Ninyi mulipokea Roho Mutakatifu wakati mulipoamini?” Nao wakamujibu: “Hapana! Hatujasikia hata kidogo kwamba kuko Roho Mutakatifu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akawauliza, Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hatta kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.