Acts 19:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu wa kike Artemi aliye mkuu, anayeabudiwa jimbo lote la Asia na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi, kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninaogopa hili litawafanya watu kuwa kinyume na biashara yetu. Lakini kuna tatizo jingine pia. Watu wataanza kufikiri kuwa hekalu la Artemi, mungu wetu mkuu halina maana. Ukuu wake utaharibiwa. Na Artemi ni mungu mke anayeabudiwa na kila mtu katika Asia na ulimwengu wote.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu mke Artemi, aliye mkuu, anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu mke Artemi, aliye mkuu, anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi, kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini linalotuogopesha si hilo tu la kwamba: Uchumi wetu utatoweka, ila hata patakatifu pa Artemi aliye mungu wetu wa kike mkuu patabezwa kuwa si kitu. Tena pataangamia ujumbe wake mkuu unaotambikiwa na watu wote wa Asia na wa ulimwengu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi, kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi kunakuwa hatari, na si kwa kazi hii yetu kuzarauliwa tu, lakini vilevile hekalu la mungu mukubwa muke, Artemi, litahesabiwa kuwa kitu bure. Na tena utukufu wake utapunguka, yeye anayeabudiwa na watu wote wa Azia na dunia nzima!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Si kwamba kazi hii yetu ina khatari ya kudharauliwa, bassi; bali na hekalu ya mungu mke aliye mkuu kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambae Asia yote pia na walimwengu wote humwtihudu.