Acts 19:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawakamata Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia waliokuwa wakisafiri na Paulo, wakakimbilia nao katika ukumbi wa maonesho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia mahali pa michezo kwa nia moja, wakiisha kuwakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paulo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mji wote ukalipuka kwa vurugu. Watu wakawakamata Gayo na Aristarko, waliotoka Makedonia waliokuwa wanasafiri na Paulo, wakawapeleka kwenye uwanja wa mji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara mji wote ukajaa ghasia, wakawakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo, watu wakakimbilia katika ukumbi wa michezo kama mtu mmoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara mji wote ukajaa ghasia. Wakawakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo, na watu wakakimbilia katika ukumbi wa michezo kama mtu mmoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia ukumbi wa michezo kwa pamoja, wakiisha kuwakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paulo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mji ukajaa machafuko, wakapiga mbio wote pamoja kwenda penye machezo, wakawakamata hapo na kuwaburura akina Gayo na Aristarko waliokuwa Wamakedonia, kwani waliandamana na Paulo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia mahali pa michezo kwa nia moja, wakiisha kuwakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paulo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Fujo ikajaa katika muji wote. Wale watu wakawakamata wanainchi wa Makedonia, Gayo na Aristarko waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo. Nao wote pamoja wakawapeleka kwa haraka katika nyumba ya makutano.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.