Acts 19:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati wa watu walikuwa na taharuki. Walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafuka-chafuka, na wengi wao hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wengi walikuwa akipiga kelele kusema hili na wengine walisema jambo jingine. Mkutano ukawa na vurugu kubwa. Watu wengi hawakujua ni kwa nini walikwenda pale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya watu walikuwa wakilia hivi na wengine vile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ule umati ulikuwa na taharuki. Wengine walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafukachafuka, na wengi wao hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo walikuwa wanapiga kelele, wengine hivi, wengine hivi. Watu waliokusanyika hapo walikuwa wamevurugika, wengi hawakujua kilichowakusanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafuka-chafuka, na wengi wao hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, mukutano ulikuwa umejaa fujo kwa sababu watu wamoja walikuwa wakilalamika na kusema hivi na wengine hivi, na wengi kati yao hawakujua hata ni kwa sababu gani walikusanyika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi: kwa maana ule mkutano umekwisha kuchafukachafuka, na walio wengi hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.