Acts 19:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkono akitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wayahudi wakamsukumia Iskanda mbele na baadhi ya watu kwenye umati ule wakampa maelekezo. Akawaashiria kwa mkono ili watulie aweze kujitetea mbele ya watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamtoa Iskanda katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskanda akawapungia mkono, akitaka kujitetea mbele ya wale watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya Wayahudi wakamshawishi mtu mmoja aliyeitwa Iskanda asimame mbele ya umati, wakamwelekeza cha kusema. Iskanda alipunga mkono wake, akijaribu kuwaeleza watu jambo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkono akitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkono akitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wayahudi wakamsukumia Aleksanda mbele na baadhi ya watu kwenye ule umati wakampa maelekezo. Akawaashiria kwa mkono ili watulie aweze kujitetea mbele ya watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wayahudi wakamsukumia Iskanda mbele na baadhi ya watu kwenye ule umati wakampa maelekezo. Akawaashiria kwa mkono ili watulie aweze kujitetea mbele ya watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamtoa Iskanda katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskanda akawapungia mkono, akitaka kujitetea mbele ya wale watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkono akitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wengine wakamshika Alekisandro, Wayuda waliyemsogeza, aje mbele. Naye Alekisandro akawapungia mkono, akataka kujikania mbele ya makutano;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamtoa Iskanda katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskanda akawapungia mkono, akitaka kujitetea mbele ya wale watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja katika mukutano wakaeleza mambo yaliyotokea kwa Alesanduro, yeye aliyesukumwa na Wayuda kwenda kusema mbele ya watu. Basi Alesanduro akainua mukono kwa kuwanyamazisha watu, kwa maana alitaka kujitetea mbele yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakatoa Iskander katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskander akawapungia mkono, akitaka kuwapa wale watu majibu.