Acts 19:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo akasema, “Ubatizo wa Yahya ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani Isa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo akasema, “Yohana aliwaambia watu wabatizwe kuonesha kuwa walidhamiria kubadili maisha yao. Aliwaambia watu kuamini katika yule atakaye kuja baada yake, naye huyo ni Yesu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonyesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo akasema, “Ubatizo wa Yahya ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Isa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Paulo aliposema: Yohana alibatiza ubatizo wa kujutisha akiwaambia watu, wamtegemee atakayekuja nyuma yake, naye ndiye Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Paulo akawaambia: “Yoane aliwabatiza wale waliogeuka toka zambi zao na kuwaambia Waisraeli kwamba wamwamini yule atakayekuja nyuma yake, naye ndiye Yesu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu.