Acts 19:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya ufalme wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akijadiliana na watu na kuwashawishi katika mambo ya ufalme wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo akaingia katika sinagogi na akazungumza kwa ujasiri. Aliendelea kufanya hivi kwa miezi mitatu. Alizungumza na Wayahudi, akijaribu kuwashawishi kukubali alichokuwa anawaambia kuhusu ufalme wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya Ufalme wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya ufalme wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akawa na majadiliano ya kuwafanya watu waamini mambo yanayohusu Ufalme wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akijadiliana na watu na kuwashawishi katika mambo ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya ufalme wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoingia nyumbani mwa kuombea, akapiga mbiu waziwazi yapata miezi mitatu, akaongeana nao mambo ya ufalme wa Mungu na kuwashinda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akiingia katika nyumba ya kuabudia na kuhubiri watu kwa uhodari. Akabishana nao juu ya habari za Ufalme wa Mungu, akitaka wazisadiki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu.