Acts 2:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
‘Mungu anasema: Katika siku za mwisho, nitaimimina Roho yangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatabiri. Vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu anasema: Siku za mwisho ndipo, itakapokuwa, niwamiminie Roho yangu wote wenye miili ya kimtu. Nao wana wenu wa kiume na wa kike watasema na kufumbua, nao vijana wenu wataona maono; nao wazee wenu wataoteshwa ndoto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
‘Mungu anasema: Katika siku za mwisho, nitashusha Roho wangu juu ya watu wote; wana wenu na wabinti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono nao wazee wenu wataota ndoto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto: