Acts 2:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Isa Al-Nasiri alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu Waisraeli, sikilizeni ninayowaambia: Mungu aliwaonesha wazi kuwa Yesu kutoka Nazareti alikuwa mtu wake. Mungu alilithibitisha hili kwa miujiza, maajabu na ishara alizotenda Yesu. Ninyi nyote mliyaona mambo haya, na mnajua hii ni kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kwa kupitia yeye, kama ninyi wenyewe mjuavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Isa Al-Nasiri alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mwenyezi Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Enyi wanaume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Enyi waume wa Kiisiraeli, yasikilizeni maneno haya! Yesu wa Nasareti alikuwa amejulikana, kwamba ametoka kwa Mungu hapo alipokuja kwenu na kufanya vya nguvu na vioja na vielekezo, tena ni Mungu aliyempa kuvifanya machoni penu, kama mnavyojua wenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ninyi wanainchi wenzangu Waisraeli, musikilize maneno haya: Yesu wa Nazareti alikuwa mutu aliyetambulishwa wazi na Mungu mbele yenu kwa njia ya vitambulisho, miujiza, na maajabu aliyofanya katikati yenu kama munavyojua ninyi wenyewe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;