Acts 2:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Daudi alisema juu yake hivi: ‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima; yuko nami upande wangu wa kulia hata sitatikisika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Daudi asema hivi kumhusu: “ ‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daudi alilisema hili kuhusu Yesu: ‘Sijasahau kuwa Bwana yu pamoja nami. Yupo hapa pembeni yangu, hivyo hakuna kinachoweza kunidhuru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Daudi alisema juu yake hivi: Nilimwona Bwana mbele yangu daima; yuko nami upande wangu wa kulia, na hivyo sitatikisika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Daudi alisema juu yake hivi: ‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima; yuko nami upande wangu wa kulia hata sitatikisika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Daudi asema kumhusu yeye: “ ‘Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Daudi asema kumhusu yeye: “ ‘Nalimwona Bwana Mwenyezi mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Daudi ataja habari zake, Nilimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kulia, nisitikisike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Daudi alisema juu yake hivi: ‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima; yuko nami upande wangu wa kulia hata sitatikisika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Dawidi anamsema: Nalimwona Bwana mbele yangu kila, nilipokuwa, kwani yuko kuumeni kwangu, nisitikisike.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mufalme Daudi alisema hivi juu yake: ‘Nilikuwa nikimwona Bwana mbele yangu saa zote; yeye ni karibu nami, kusudi nisitikisike.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana Daud amtaja khabari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko mkono wangu wa kuume, nisitikisike.