Acts 2:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipokwisha pandishwa na kuwekwa na Mungu upande wake wa kulia, akapokea kutoka kwake Baba yule Roho Mtakatifu ambaye alituahidi, ametumiminia huyo Roho. Hicho ndicho mnachoona sasa na kusikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi yeye ametukuzwa hadi mkono wa kuume wa Mungu, na amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu wa Mungu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alichukuliwa juu mbinguni. Na sasa ameketi upande wa kulia wa Mungu. Baba amempa Roho Mtakatifu, kama alivyoahidi. Hivyo Yesu amemimina huyo Roho Mtakatifu na hiki ndicho mnachoona na kusikia
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliinuliwa juu mpaka upande wa kulia wa Mungu, akapokea kutoka kwa Baba ile zawadi aliyoahidi yaani Roho Mtakatifu; na mnachoona sasa na kusikia ni mmiminiko wa huyo Roho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipokwisha pandishwa na kuwekwa na Mungu upande wake wa kulia, akapokea kutoka kwake Baba yule Roho Mtakatifu ambaye alituahidi, ametumiminia huyo Roho. Hicho ndicho mnachoona sasa na kusikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho wa Mwenyezi Mungu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yeye, akiisha kupandishwa hadi mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipokwisha pandishwa na kuwekwa na Mungu upande wake wa kulia, akapokea kutoka kwake Baba yule Roho Mtakatifu ambaye alituahidi, ametumiminia huyo Roho. Hicho ndicho mnachoona sasa na kusikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipokwisha kupazwa juu, akae kuumeni kwa Mungu, akapata ruhusa kwa Baba yake kukitimiza kiagio cha Roho Mtakatifu, akaimimina yiyo hiyo, ninyi mnayoiona, tena mnayoisikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kisha kunyanyuliwa aikae na mamlaka kwa kuume kwa Mungu Baba yake, yeye akamupa Roho Mutakatifu aliyeahidiwa. Naye akamushusha juu yetu, sawa vile munavyojionea na kusikia wenyewe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.