Acts 2:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waliuza mashamba yao na vitu walivyomiliki, kisha wakatoa fedha na kuwapa wenye kuhitaji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, wakamgawia kila mtu kwa kadiri alivyokuwa anahitaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kulingana na haja ya kila mmoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakauza mali zao navyo vyote, walivyokuwa navyo, wakavigawia wote, kila mtu apate, kama alivyokosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliuzisha mali zao na vyote walivyokuwa navyo na kugawanya kati yao kufuatana na mahitaji ya kila mutu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja.