Acts 2:47 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waamini walimsifu Mungu na waliheshimiwa na watu wote. Watu wengi zaidi waliokolewa kila siku, na Bwana alikuwa akiwaongeza kwenye kundi lao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa kwa wale watu waliokuwa wakiokolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakimsifu Mwenyezi Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana Mwenyezi akawaongeza waumini wale waliokuwa wakiokolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamsifu Mungu, wakawapendeza watu wote. Naye Bwana akawaongeza kila siku na kutia papo hapo wenye kuokoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walisifu Mungu na kufurahiwa na watu wote. Na kila siku Bwana aliongeza katika kundi la waamini watu waliokuwa wakiokolewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.