Acts 20:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi kavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tukatangulia kwenye meli, tukasafiri kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Alikuwa amefanya utaratibu huu kwa sababu alikuwa akienda huko kwa miguu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulimtangulia Paulo, tukatweka tanga kwenda Asso, tulipanga kumkuta huko. Alitwambia tufanye hivi kwa sababu alitaka kusafiri kwa nchi kavu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi kavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi kavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tukaingia melini tukasafiri kwa njia ya bahari mpaka Aso ambako ndiko tungempakia Paulo, alikuwa amepanga hivyo maana alitaka kufika kwa miguu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tukatangulia melini tukasafiri mpaka Aso ambako tungempakia Paulo. Alikuwa amepanga hivyo kwa maana alitaka kufika kwa miguu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukakabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimia kwenda kwa miguu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi kavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sisi tulitangulia kuingia chomboni, tukatweka kwenda Aso; ndiko, tulikotaka kumpakia Paulo. Kwani alikuwa ametuagiza hivyo; mwenyewe alitaka kufika huko kwa miguu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi tulitangulia tukaingia ndani ya chombo na kusafiri kwenda Asosi. Kule tulipaswa kumutwaa Paulo sawa alivyotuagiza, kwa maana alikuwa amekusudia kwenda kule kwa miguu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukasafiri hatta Asso, tukikusudia kumpokea Paolo huko: kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe akiazimu kwenda kwa miguu.