Acts 20:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo alikuwa amekusudia kuendelea na safari kwa meli bila kupitia Efeso ili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kwa sikukuu ya Pentekoste kama ingewezekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi huko jimbo la Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste kama ingewezekana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo alikwisha amua kutosimama Efeso. Hakutaka kukaa Asia kwa muda mrefu. Alikuwa anaharakisha kwa sababu alitaka ikiwezekana awe Yerusalemu siku ya Pentekoste.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo alikuwa amekusudia kuendelea na safari kwa meli bila kupitia Efeso ili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kwa sikukuu ya Pentekoste kama ingewezekana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo alikuwa amekusudia kuendelea na safari kwa meli bila kupitia Efeso ili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kwa sikukuu ya Pentekoste kama ingewezekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi huko sehemu za Asia, kwa sababu alikuwa anatamani kama ikiwezekana kufika Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi huko sehemu za Asia, kwa sababu alikuwa anatamani kama ikiwezekana kufika Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu Paulo alikusudia kusafiri pasipo kupitia Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo alikuwa amekusudia kuendelea na safari kwa meli bila kupitia Efeso ili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kwa sikukuu ya Pentekoste kama ingewezekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Paulo alitaka kupita Efeso kwa chombo, asipate kukawia katika Asia, maana alikwenda mbiombio, kwa sababu alitaka ikiwezekana, kuila sikukuu ya Pentekote huko Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Paulo alikuwa amekusudia kupita Efeso kwa chombo pasipo kuezeka kule, kusudi asikawie katika jimbo la Azia. Kwa maana alikuwa na haraka ya kufika Yerusalema mbele ya siku ya Pentekoste kama ikiwezekana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu Paolo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia: kwa maana alikuwa akifanya haraka, akitaka kuwahi Yerusalemi siku ya Pentekote, kama ikiwezekana.