Acts 20:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa-mwitu wakali watakuja kati yenu, ambao hawatalihurumia kundi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninafahamu ya kwamba nikishaondoka, baadhi ya watu watakuja kwenye kundi letu. Watakuwa kama mbwa mwitu na watajaribu kuwaangamiza kondoo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Najua kwamba baada mimi kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi najua: Nitakapokwisha kuondoka, wataingia chui wakali kwenu wasiowaonea huruma wao wa kikundi hiki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninajua kwamba nyuma ya kuondoka kwangu, imbwa wakali wa pori wataingia katikati yenu, nao hawatahurumia kundi lile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa za mwitu wakali watakuja kwenu, wasiliachie kundi: