Acts 20:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Kwa sababu baadhi ya Wayahudi walikuwa wamepanga njama dhidi yake alipokuwa karibu kusafiri kwa meli kwenda Siria, aliamua kurudi kupitia Makedonia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
na alikaa huko kwa miezi mitatu. Alipokuwa tayari kutweka tanga kwenda Shamu, baadhi ya Wayahudi walikuwa wanapanga kitu kinyume naye. Hivyo aliamua kurudi nyuma kwenda Shamu kupitia Makedonia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya bahari kwenda Shamu, kwa sababu Wayahudi walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yake, aliamua kurudi kwa kupitia njia ya Makedonia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya bahari kwenda Shamu, kwa sababu Wayahudi walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yake, aliamua kurudi kupitia njia ya Makedonia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimbwi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akakaa huko miezi mitatu. Alipotaka kuingia chomboni, aende Ushami, Wayuda walimlia njama. Kwa hiyo akapendezwa kurudi na kupita Makedonia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kukaa kule kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa tayari kuvuka na chombo kwenda katika inchi ya Suria, akapata habari kwamba Wayuda walimufanyia shauri baya. Kwa hiyo akakusudia kurudia, akipitia Makedonia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, Wayahudi wakamfanyyia vitimbi, alipotaka kwenda Sham kwa njia ya bahari: bassi akaazimu kurejea kwa ujia ya Makedonia.