Acts 20:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kila jambo nimewaonesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Isa mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daima niliwaonesha kwamba mnapaswa kufanya kazi nilivyofanya na kuwasaidia wadhaifu. Niliwafundisha kukumbuka maneno ya Bwana Yesu aliyosema, ‘Ni baraka kuu kutoa kuliko kupokea.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kila jambo nililofanya, nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni baraka zaidi kutoa kuliko kupokea.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Isa mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwangu mimi nimewaonyesha yote, ya kuwa imetupasa kusumbukia kazi vivyo hivyo, tupate kuwasaidia wanyonge, tukiyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, aliyoyasema mwenyewe: Kumpa mtu huna upato kuliko kupewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mambo hayo yote niliyofanya, nimewaonyesha mufano kwamba tunapaswa kusumbuka vile na kazi kwa kuwasaidia wasiojiweza, tukikumbuka maneno haya Bwana Yesu mwenyewe aliyosema: ‘Ni heri kutoa kuliko kupewa.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea.