Acts 20:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi, baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwa muda wa juma moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sisi tukasafiri kwa meli kwa siku tano kutoka Filipi baada ya siku za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, nasi tukaungana na wengine huko Troa, ambako tulikaa kwa siku saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya Siku kuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu tulitweka tanga kutoka katika mji wa Filipi. Tuliwakuta watu hawa katika mji wa Troa siku tano baadaye na tulikaa pale kwa siku saba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi, baada ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwa muda wa juma moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi, baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwa muda wa juma moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sisi tukasafiri kwa njia ya bahari kwa siku tano kutoka Filipi baada ya siku za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, nasi tukaungana na wengine huko Troa, ambako tulikaa kwa siku saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sisi tukasafiri kwa njia ya bahari kwa siku tano kutoka Filipi baada ya siku za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, nasi tukaungana na wengine huko Troa, ambako tulikaa kwa siku saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, baada ya safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi, baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwa muda wa juma moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za mikate isiyotiwa chachu zilipopita, nasi tukatweka, tukaondoka Filipi, tukawafikia huko Tiroa siku ya tano, tukaa huko siku saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini nyuma ya sikukuu ya Mukate Usiotiwa Chachu, sisi tukaondoka katika muji Filipi kwa njia ya chombo. Na kisha safari ya siku tano tukawakuta Troa, nasi tukakaa kule kwa muda wa siku saba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisi tukatweka baada ya siku ya mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filippi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.