Acts 20:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kijana mmoja aitwaye Eutuko alikuwa ameketi dirishani wakati Paulo alipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutuko alianza kusinzia kidogokidogo na hatimaye usingizi ukambana, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu. Wakamwokota amekwisha kufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kijana mmoja jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akihubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamchukua akiwa amekufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa amekaa dirishani aliyeitwa Eutiko. Paulo aliendelea kuzungumza, na Eutiko alianza kuchoka na kusikia ungungizi. Mwishowe alisinzia na kuanguka. Alianguka chini, nje kutoka ghorofa ya tatu. Watu walipokwenda kumnyenyua alikuwa amekwisha kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kijana mmoja aitwaye Eutuko alikuwa ameketi dirishani wakati Paulo alipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutuko alianza kusinzia kidogokidogo na hatimaye usingizi ukambana, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu. Wakamwokota amekwisha kufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kijana mmoja aitwaye Eutuko alikuwa ameketi dirishani wakati Paulo alipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutuko alianza kusinzia kidogokidogo na hatimaye usingizi ukambana, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu. Wakamwokota amekwisha kufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kijana mmoja jina lake Eutiko, aliyekuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akiendelea kuhubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamwinua akiwa amekufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kijana mmoja jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akihubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamwinua akiwa amekufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka ghorofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kijana mmoja aitwaye Eutuko alikuwa ameketi dirishani wakati Paulo alipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutuko alianza kusinzia kidogokidogo na hatimaye usingizi ukambana, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu. Wakamwokota amekwisha kufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mlikuwa na kijana, jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, akasinzia mno. Paulo alipofuliza kusema, akashindwa na usingizi, akaanguka toka dari ya tatu mpaka chini, akainuliwa amekufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kijana mumoja, aliyeitwa Eutiko, alikuwa akiikaa kwenye dirisha. Na kwa muda ule murefu Paulo alipofundisha, Eutiko akaanza kusinziasinzia na kwa mwisho akawezwa na usingizi na akaanguka chini toka kwenye gorofi ya tatu. Walipomunyanyua alikuwa amekwisha kufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kijana mmoja, jina lake Eutuko, ameketi dirishani, akalemewa na usingizi, akaanguka toka orofa ya tatu: akainuliwa amekwisha kufa.