Acts 21:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka Kosi. Kesho yake tulifika Rode, na kutoka huko tulikwenda Patara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tulipokwisha kujitenga nao, tukasafiri kwa meli moja kwa moja hadi Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo, na kutoka huko tukaenda Patara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na kuabiri, tukafika Kosi kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya kuwaaga wazee tulitweka tanga moja kwa moja kwenda kwenye kisiwa cha Kosi. Siku iliyofuata tulikwenda kisiwa cha Rhode na kutoka pale tulikwenda Patara.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka Kosi. Kesho yake tulifika Rodo, na kutoka huko tulikwenda Patara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka Kosi. Kesho yake tulifika Rode, na kutoka huko tulikwenda Patara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tulipokwisha kujitenga nao, tukaanza safari kwa njia ya bahari moja kwa moja mpaka Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukaenda Patara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tulipokwisha kujitenga nao, tukaanza safari kwa njia ya bahari moja kwa moja mpaka Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukaenda Patara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na kuabiri, tukafika Kosi kwa tanga moja, na kesho yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka Kosi. Kesho yake tulifika Rode, na kutoka huko tulikwenda Patara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tulipokwisha kuagana nao tukatweka na kukielekeza chombo kwenda Ko kwa tanga moja; tulipofika, kesho yake tukaenda hapo Rodo; toka hapo tukafika Patara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na kuabiri, tukafika Kosi kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulipokwisha kuagana nao, tukasafiri ndani ya chombo na kwenda mara moja mpaka kwenye kisanga cha Kosi. Kesho yake tukafika katika muji Rodo, na kutoka kule tukafika katika muji Patara.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
IKAWA tulipokwisha kujitenga nao ua kutweka, tukafika Koos kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,