Acts 21:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na gharama zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba wewe binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya sheria za Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jiunge na watu hawa, mfanye utaratibu wa ibada ya kujitakasa pamoja nao, na ulipe gharama ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unaishika sheria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wachukue watu hawa walio pamoja nawe na ushiriki katika ibada ya utakaso. Lipia gharama zao ili wanyoe nywele za vichwa vyao. Hili litathibitisha kwa kila mmoja kuwa mambo waliyosikia kuhusu wewe si sahihi. Watajua kuwa wewe mwenyewe unaitii Sheria ya Musa katika maisha yako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na gharama zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba wewe binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya Sheria za Mose.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na gharama zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba wewe binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya sheria za Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jiunge na watu hawa, mfanye utaratibu wa ibada ya kujitakasa pamoja nao na ulipe gharama ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unaishika sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jiunge na watu hawa, mfanye utaratibu wa ibada ya kujitakasa pamoja nao, na ulipe gharama ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unaishika sheria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na gharama zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba wewe binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya sheria za Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wachukue hao ujieue pamoja nao, uwalipie, wanyolewe vichwa! Hivyo wote watatambua, ya kuwa waliyoambiwa kwa ajili yako ni uwongo tu, ya kuwa wewe mwenyewe unaendelea na kuyashika Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenda ujiunge na watu wale katika ibada ya utakaso, nawe uwalipie malipo yanayoamuriwa kusudi wapate kunyolewa. Hivi watu wote watajua kwamba habari zile walizoambiwa juu yako zilikuwa za uongo mutupu. Na zaidi ya hii watajua kwamba unafuata Sheria ya Musa katika maisha yako.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Chukua watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia illi wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa khabari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika sharia.