Acts 21:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa waumini, tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: Wasile chochote kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kuhusu wale watu wa Mataifa walioamini, tumewaandikia uamuzi wetu: kwamba wajitenge na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tumekwisha watumia barua waamini wasio Wayahudi kuwaambia ambayo hawapaswi kufanya: ‘Wasile chakula kilichotolewa kwa sanamu. Wasile nyama inayotokana na wanyama walionyongwa au nyama zilizo na damu ndani yake. Wasijihusishe na uzinzi.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa waumini, tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: wasile chochote kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa waumini, tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: wasile chochote kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kuhusu wale watu Mataifa walioamini tumewaandikia uamuzi wetu kwamba wajitenge na kitu cho chote kilichotolewa sadaka kwa sanamu na damu au kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa kunyongwa, tena wajitenge na uasherati.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kuhusu wale watu wa Mataifa walioamini, tumewaandikia uamuzi wetu: kwamba wajitenge na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kuhusu watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa waumini, tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: Wasile chochote kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa ajili ya wamizimu walioanza kumtegemea Bwana tumewaandikia, tulivyopatana ya kwamba, waushike mzio wa nyama za tambiko na wa damu na wa nyamafu na wa ugoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa ngambo ya watu wa mataifa mengine walioamini, tumekwisha kuwaandikia juu ya mambo tuliyoamua. Tumewaamuru kwamba wasikule vyakula vilivyotolewa kwa kutambikia sanamu; wasikule damu wala nyamafu; na waepuke uasherati.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa khabari za watu wa mataifa walioamini, tumekwisha kutoa hukumu yetu, wsio wasishike neno linginelo illa kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongwa, na uasharati.