Acts 21:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri hadi Siria. Tukatia nanga katika bandari ya Tiro, ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulitweka tanga na kusafiri karibu na kisiwa cha Kipro. Tuliweza kukiona upande wa kaskazini, lakini hatukusimama. Tulisafiri mpaka katika jimbo la Shamu. Tulisimama Tiro kwa sababu meli ilitakiwa kupakua mizigo yake pale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulipokuona kule Kipuro tukakuacha kushotoni, tukaendelea mpaka Ushami, tukashukia Tiro; kwani ndiko, chombo kilikoagiziwa kuipakua mizigo yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulipoanza kuona kisanga cha Kipuro, tukikiacha kwa upande wa kusini na kuelekea katika jimbo la Suria. Tukaezeka kwenye kivuko cha Tiro, kwa maana ni pale chombo kilipaswa kupakuliwa mizigo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.