Acts 21:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari, akalikabili lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara yule jemadari akachukua maafisa wengine wa jeshi pamoja na askari, wakakimbia kwenye ule umati wa watu. Wale watu waliokuwa wakifanya ghasia walipomwona yule jemadari na askari wakija, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara hiyo hiyo kamanda alikimbilia mahali ambako umati wa watu ulikuwa umekusanyika, aliwachukua baadhi ya maofisa wa jeshi na askari. Watu walipomwona kamanda na askari wake waliacha kumpiga Paulo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari, akalikabili lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari, akalikabili lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara yule jemadari akachukua maafisa wengine wa jeshi pamoja na maaskari wakakimbilia kwenye ile ghasia, wale watu waliokuwa wakifanya ghasia walipomwona yule jemadari na askari wakija, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara yule jemadari akachukua maafisa wengine wa jeshi pamoja na askari wakakimbilia kwenye ile ghasia, wale watu waliokuwa wakifanya ghasia walipomwona yule jemadari na askari wakija, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara akatwaa askari na maofisa, akawaendea mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari, akalikabili lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara hiyo akachukua askari na wakubwa wao, akashuka kwao mbiombio. Wale walipomwona mkuu na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja akatwaa waaskari pamoja na wakubwa wao na kwenda nao haraka pale watu walipokusanyika. Nao walipomwona huyo mwongozi pamoja na waaskari wake wakaacha kumupiga Paulo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra hiyo akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paolo.