Acts 21:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya watu katika umati ule wakapiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya taharuki, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya watu pale walipiga kelele wakisema kitu hiki na wengine walisema kingine. Kwa sababu ya kuchanganyikiwa huku na kelele kamanda hakujua ukweli kuhusu kilichotokea. Hivyo akawaambia askari wamchukue Paulo mpaka kwenye jengo la jeshi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya watu katika ule umati wakapiga kelele, hawa wakisema hili na wengine wakisema lile. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya watu katika ule umati wakapiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu kwa hivyo, walivyokuwa wengi, wengine wakapiga kelele hivyo, wengine hivyo. Asipoweza kuyatambua yaliyo kweli kwa ajili ya makelele akaagiza, apelekwe bomani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamoja katika makutano walikuwa wakilalamika na kusema hivi, na wengine hivi. Basi kwa kuwa yule kiongozi hakuweza kupata jibu kamili kwa sababu ya makelele, akaamuru kwamba wamupeleke Paulo ndani ya upango wa waaskari.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Bassi alipokuwa hawezi kupata hakika ya khabari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.