Acts 21:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika kumbeba kwa sababu ya fujo za watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo alipofika penye ngazi, ilibidi askari wambebe juu juu kwa sababu fujo za umati ule wa watu zilikuwa kubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Paulo alipofika darajani ilikuwa kuchukuliwa na askari kwa sababu ya nguvu ya makutano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Umati wote ulikuwa unawafuata. Askari walipofika kwenye ngazi ilibidi wambebe Paulo. Walifanya hivi ili kumlinda, kwa sababu watu walikuwa tayari kumwumiza. Watu walikuwa wanapiga kelele wakisema, “Auawe!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika kumbeba kwa sababu ya fujo za watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika kumbeba kwa sababu ya fujo za watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo alipofika penye ngazi, ilibidi maaskari wambebe juu juu kwa sababu fujo za ule umati wa watu zilikuwa kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo alipofika penye ngazi, ilibidi askari wambebe juu juu kwa sababu fujo za ule umati wa watu zilikuwa kubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Paulo alipofika darajani ilikuwa kuchukuliwa na askari kwa sababu ya nguvu ya makutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika kumbeba kwa sababu ya fujo za watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika pa kupandia akachukuliwa na askari, wamkingie ukorofi wa watu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Paulo alipofika darajani ilikuwa kuchukuliwa na askari kwa sababu ya nguvu ya makutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Paulo alipofika kwenye ngazi, waaskari walilazimishwa kumubeba kwa sababu makutano yalitomboka sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi alipolika darajani ilikuwa yeye kuchukuliwa na askari kwa sababu ya jeuri ya makutano.