Acts 21:36 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana watu kundi kubwa walimfuata wakipiga kelele, “Mwulie mbali!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati wa watu waliofuata waliendelea kupaza sauti na kusema, “Mwondoe huyu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, na kusema, Mwondoe huyu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana kundi kubwa la watu walimfuata wakipiga kelele, “Muulie mbali!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana watu kundi kubwa walimfuata wakipiga kelele, “Mwulie mbali!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ule umati wa watu walikuwa wakifuata wakiendelea kupiga kelele wakisema, “Mwondoe huyu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umati wa watu ulikuwa ukifuata ukiendelea kupiga kelele ukisema, “Mwondoe huyu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, na kusema, Na aondolewe mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana watu kundi kubwa walimfuata wakipiga kelele, “Mwulie mbali!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani watu wengi mno walimfuata wakipiga kelele kwamba: Mwondoe huyu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, na kusema, Mwondoe huyu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana wote walimufuata nyuma wakilalamika: “Auawe!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, Mwondoe huyu.