Acts 21:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba mkuu wa jeshi akisema, “Naweza kukuambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akamjibu, “Je, unajua Kigiriki?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu Paulo alipokaribia kuingizwa kwenye ngome ya jeshi, akamwambia yule jemadari, “Je, naweza kukuambia jambo moja?” Yule jemadari akamjibu, “Je, unajua Kiyunani?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kiyunani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Askari walipokuwa tayari kumwingiza Paulo kwenye jengo la jeshi, Paulo alimwuliza kamanda akasema, “Je, ninaweza kukwambia kitu?” Kamanda akasema, “Kumbe, unaongea Kiyunani?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba mkuu wa jeshi akisema, “Naweza kukwambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akamjibu, “Je unajua Kigiriki?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba mkuu wa jeshi akisema, “Naweza kukuambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akamjibu, “Je, unajua Kigiriki?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu Paulo alipokaribia kuingizwa kwenye ngome ya jeshi, akamwambia yule jemadari, “Je, naweza kukuambia jambo moja?” Yule jemadari akamjibu, “Je, unajua Kiyunani?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu Paulo alipokaribia kuingizwa kwenye ngome ya jeshi, akamwambia yule jemadari, “Je, naweza kukuambia jambo moja?” Yule jemadari akamjibu, “Je, unajua Kiyunani?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kigiriki?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba mkuu wa jeshi akisema, “Naweza kukuambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akamjibu, “Je, unajua Kigiriki?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipotaka kumwingiza bomani, Paulo akamwambia mkuu wa askari: Niko na ruhusa kukuambia neno? Naye aliposema: Unajua Kigriki?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kiyunani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari walipotaka kumwingiza Paulo katika upango, akamwuliza mukubwa wa kundi la waaskari: “Unaweza kuniruhusu kukuambia neno moja?” Yule mukubwa wa kundi la waaskari akamwuliza: “Unajua Kigriki?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Paolo alipokuwa anaingizwa ndani ya ngome, akamwambia jemadari, Nina rukhusa nikuambie neno? Nae akasema, Je! unajua Kiyunani?