Acts 22:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtu mmoja mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona. Alizishika sana sheria zetu, na aliheshimiwa sana na Wayahudi walioishi huko Dameski.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwepo mtu mmoja katika mji wa Dameski aliyeitwa Anania. Mtu huyu alikuwa mcha Mungu na aliitii Sheria ya Musa na Wayahudi wote walioishi kule walimheshimu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii Sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtu mmoja Mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona, aliyeshika sana sheria zetu, na ambaye aliheshimiwa sana na Wayahudi waliokuwa wakiishi huko Dameski,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtu mmoja mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona. Alizishika sana sheria zetu, na aliheshimiwa sana na Wayahudi waliokuwa wakiishi huko Dameski.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na mtu, jina lake Anania, ni mwenye kuyashika Maonyo yote, kama wanavyomshuhudia Wayuda wote wanaokaa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kule Damasiki kulikuwa mutu mumoja aliyeitwa Anania, mutu aliyeogopa Mungu na mwenye kushika Sheria yetu. Aliheshimiwa sana na Wayuda wote waliokaa kule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.