Acts 22:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimwona Bwana akiniambia, ‘Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nikamwona Bwana Isa akiniambia, ‘Harakisha utoke Yerusalemu upesi, maana hawataukubali ushuhuda wako kunihusu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika habari zangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilimwona Yesu, naye akaniambia, ‘Haraka, ondoka Yerusalemu sasa hivi! Watu hapa hawataukubali ukweli unaowaambia kuhusu mimi.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilimwona Bwana akiniambia: Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa binadamu hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimwona Bwana akiniambia, ‘Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nikamwona Yesu akiniambia, ‘Harakisha utoke Yerusalemu upesi, maana hawataukubali ushuhuda wako kunihusu mimi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nikamwona Bwana Isa akiniambia, ‘Harakisha utoke Yerusalemu upesi, maana hawataukubali ushuhuda wako kunihusu mimi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako kuhusu habari zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilimwona Bwana akiniambia, ‘Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nikamwona, naye akaniambia; Piga mbio, utoke upesi Yerusalemu! Kwani hawatakupokea, ukinishuhudia mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika habari zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikamwona Bwana, naye akaniambia: ‘Fanya haraka uondoke upesi katika muji huu Yerusalema kwa sababu watu wake hawatakubali ushuhuda utakaoutoa juu yangu.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nikamwona akiniambia, Hima, toka katika Yerusalemi upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika khabari zangu.