Acts 22:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpaka hapa, wale watu walikuwa wanamsikiliza, lakini aliposema maneno haya, walianza kusema kwa sauti kubwa, “Mwondoe duniani! Mtu wa namna hiyo hastahili kuishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati ule wa watu wakamsikiliza Paulo hadi aliposema neno hilo, ndipo wakapaza sauti zao na kupiga kelele wakisema, “Mwondoeni duniani, hafai kuishi!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi, kwa maana haifai aishi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu waliacha kusikiliza Paulo aliposema jambo hili la mwisho. Walipasa sauti wote, wakisema, “Mwondosheni mtu huyu! Hastahili kuishi katika dunia hii tena.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mpaka hapa, wale watu walikuwa wanamsikiza, lakini aliposema maneno haya, walianza kusema kwa sauti kubwa, “Mwondoe duniani! Mtu wa namna hiyo hastahili kuishi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpaka hapa, wale watu walikuwa wanamsikiliza, lakini aliposema maneno haya, walianza kusema kwa sauti kubwa, “Mwondoe duniani! Mtu wa namna hiyo hastahili kuishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ule umati wa watu wakamsikiliza Paulo mpaka aliposema neno hilo, ndipo wakapaza sauti zao na kupiga kelele wakisema, “Mwondoeni duniani, hafai kuishi!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ule umati wa watu wakamsikiliza Paulo mpaka aliposema neno hilo, ndipo wakapaza sauti zao na kupiga kelele wakisema, “Mwondoeni duniani, hafai kuishi!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi, kwa maana haifai aishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpaka hapa, wale watu walikuwa wanamsikiliza, lakini aliposema maneno haya, walianza kusema kwa sauti kubwa, “Mwondoe duniani! Mtu wa namna hiyo hastahili kuishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wale waliomsikiliza mpaka neno hili walipopaza sauti wakisema: Mwondoe huyu nchini! Kwani haimpasi kuwapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi, kwa maana haifai aishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makutano walimusikiliza Paulo mpaka aliposema maneno yale. Kisha wakasema kwa nguvu: “Mumuteketeze mutu huyu! Mumwue, kwa maana hastahili kuishi!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika inchi, kwa maana haifai aishi.