Acts 22:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini walipokwisha mfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwuliza jemadari mmoja aliyesimama hapo, “Je, ni halali kwenu kumpiga viboko raia wa Roma kabla hajahukumiwa?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wampige mijeledi, Paulo akamwambia kiongozi wa askari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, “Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumpiga mtu ambaye ni raia wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Askari walipokuwa wanamfunga Paulo, wakijiandaa kumpiga alimwuliza ofisa wa jeshi, “Je, mna haki ya kumpiga raia wa Rumi ambaye hajathibitika kuwa na hatia?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini walipokwisha mfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwuliza jemadari mmoja aliyesimama hapo, “Je, ni halali kwenu kumpiga viboko raia wa Roma kabla hajahukumiwa?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini walipokwisha mfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwuliza jemadari mmoja aliyesimama hapo, “Je, ni halali kwenu kumpiga viboko raia wa Roma kabla hajahukumiwa?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia kiongozi wa maaskari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, “Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumchapa mtu ambaye ni raia wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia kiongozi wa askari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, “Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumchapa mtu ambaye ni raiya wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule ofisa aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye bado hajakuhumiwa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini walipokwisha mfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwuliza jemadari mmoja aliyesimama hapo, “Je, ni halali kwenu kumpiga viboko raia wa Roma kabla hajahukumiwa?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipomfunga kwa mikanda, apigwe, Paulo akamwambia bwana askari aliyesimama hapo: Je? Mko na ruhusa kupiga mtu aliye Mroma, asipohukumiwa kwanza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini walipokwisha kumufunga Paulo na kamba kusudi wamupige, yeye akamwambia jemadari mumoja aliyekuwa pale: “Sheria inawaruhusu kumupiga mwanainchi wa Roma, ingawa hajahukumiwa bado?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paolo akamwambia akida aliyesimama karibu, Je! ni halali kumpiga mtu Mrumi nae hajahukumiwa bado?