Acts 22:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu ambao walikuwa tayari kumchunguza Paulo walitoweka mara. Hata yule mkuu wa jeshi aliogopa alipojua kwamba Paulo ni raia wa Roma na kwamba alikuwa amekwisha mfunga minyororo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka, naye yule jemadari akaingiwa na hofu alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raia wa Rumi, kwa minyororo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari naye akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ghafla watu waliokuwa wanajiandaa kumwuliza maswali Paulo waliondoka. Kamanda aliogopa kwa sababu alikuwa ameshamfunga Paulo kwa minyororo na ni raia wa Rumi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale watu ambao walikuwa tayari kumchunguza Paulo walitoweka mara. Hata yule mkuu wa jeshi aliogopa alipojua kwamba Paulo ni raia wa Roma na kwamba alikuwa amekwisha mfunga minyororo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu ambao walikuwa tayari kumchunguza Paulo walitoweka mara. Hata yule mkuu wa jeshi aliogopa alipojua kwamba Paulo ni raia wa Roma na kwamba alikuwa amekwisha mfunga minyororo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raia wa Rumi kwa minyororo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka, naye yule jemadari akaingiwa na hofu alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raiya wa Rumi, kwa minyororo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari naye akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale watu ambao walikuwa tayari kumchunguza Paulo walitoweka mara. Hata yule mkuu wa jeshi aliogopa alipojua kwamba Paulo ni raia wa Roma na kwamba alikuwa amekwisha mfunga minyororo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo wale waliotaka kumwuliza kwa mapigo wakamwacha. Naye mkuu wa kikosi akaogopa alipotambua, ya kuwa ni Mroma, kwani yeye alimfunga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari naye akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja wale waliotaka kumusambisha kwa kumupiga fimbo wakamwacha. Yule mukubwa wa jeshi akaogopa alipotambua kwamba Paulo ni mwanainchi wa Roma, na kwamba alikuwa anamufunga na minyororo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari nae akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.