Acts 22:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu. Miguuni mwa Gamalieli, nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, na nikawa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama nyote mlivyo leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Mimi ni Myahudi, nilizaliwa katika mji wa Tarso katika jimbo la Kilikia. Nilikulia hapa katika mji huu. Nilikuwa mwanafunzi wa Gamalieli ambaye kwa umakini alinifundisha kila kitu kuhusu sheria ya baba zetu. Daima nimekuwa na shauku ya kumheshimu Mungu, sawa na ninyi nyote hapa leo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti Sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama ninyi wenyewe mlivyo hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu, miguuni mwa Gamalieli. Nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, nikiwa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama kila mmoja wenu alivyo leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu. Miguuni mwa Gamalieli, nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, na nikawa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama kila mmoja wenu alivyo leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Mimi ni mtu wa Kiyuda, nimezaliwa Tarso katika nchi ya Kilikia. Nikalelewa humu mjini, nikakaa miguuni pa Gamalieli na kufundishwa Maonyo ya baba zetu kwa uangalifu wote. Nikajipingia kumfanyia Mungu kazi, kama nanyi nyote leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mimi ni Muyuda, nimezaliwa Tarso, katika jimbo la Kilikia, lakini nililelewa katika muji huu wa Yerusalema. Mimi nilikuwa mwanafunzi wa Gamalieli, na alinifundisha namna ya kufuata kabisa Sheria ya babu zetu. Nikajitolea kabisa kwa kutumikia Mungu kama vile ninyi wote munavyofanya leo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi: