Acts 22:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, nilipokuwa njiani karibu na kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwanga mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nilipokuwa njiani kuelekea Dameski, yapata saa sita mchana, ghafula nuru kubwa kutoka mbinguni ikanimulika kotekote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kitu fulani kilinitokea nikiwa njiani kwenda Dameski. Ilipokuwa inakaribia mchana na nilikuwa karibu na mji wa Dameski. Ghafla mwanga kutoka mbinguni ulining'aria kunizunguka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Basi, nilipokuwa njiani karibu kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, nilipokuwa njiani karibu na kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwanga mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nilipokuwa njiani kuelekea Dameski, yapata saa sita mchana, ghafula nuru kubwa kutoka mbinguni ikanimulika kote kote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nilipokuwa njiani kuelekea Dameski, yapata saa sita mchana, ghafula nuru kubwa kutoka mbinguni ikanimulika kotekote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafla nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, nilipokuwa njiani karibu na kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwanga mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nilipokwenda na kufika karibu ya Damasko, ilipokuwa saa sita ya mchana, mara palitoka mwanga mkubwa mbinguni, ukanimulikia pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Nilipokuwa katika safari karibu kufika Damasiki, yapata saa sita ya muchana, kwa rafla mwangaza mukubwa toka mbinguni ukanizunguka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhdhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.