Acts 23:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa basi, nyinyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumwua hata kabla hajafika karibu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa basi, wewe pamoja na Baraza la Wayahudi mwombeni jemadari amlete Paulo mbele yenu kwa kisingizio cha kutaka taarifa sahihi zaidi kuhusu kesi yake. Nasi tuko tayari kumuua kabla hajafika hapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunataka mfanye hivi: Mtumieni kamanda ujumbe kutoka kwenu na baraza kuu. Mwambieni mnamtaka amlete Paulo kwenu. Semeni kwamba mnataka kumwuliza maswali zaidi, tutamwua akiwa njiani kuja hapa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa basi, ninyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumuua hata kabla hajafika karibu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa basi, nyinyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumwua hata kabla hajafika karibu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo basi, wewe pamoja na baraza, inawapasa mumjulishe jemadari ili amtelemshe Paulo kwenu, mjifanye kama mnataka kufanya uchunguzi wa kina zaidi wa shauri lake. Nasi tuko tayari kumwua kabla hajafika hapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo basi, wewe pamoja na baraza, inawapasa mkamjulishe jemadari ili amteremshe Paulo kwenu, mjifanye kama mnataka kufanya uchunguzi wa kina zaidi wa shauri lake. Nasi tuko tayari kumuua kabla hajafika hapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tuko tayari kumwua kabla hajakaribia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa basi, nyinyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumwua hata kabla hajafika karibu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa ninyi wakuu nyote, mmweleze mkuu wa kikosi, amshushe kesho kwenu, kwamba mnataka kutambua kwa welekevu, mambo yake yalivyo. Lakini sisi tuko tayari kumwua, akiwa hajawafikia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi sasa, ninyi pamoja na Baraza Kubwa mumwombe jemadari awaletee Paulo, mukimwambia tu kwamba munataka kuchunguza vizuri zaidi maneno yake. Na sisi tuko tayari kumwua mbele hajafika hapa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua khabari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.