Acts 23:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mtoto wa ndugu yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia kuhusu njama hiyo, alienda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mpwaye Paulo aliusikia mpango huu. Alikwenda kwenye jengo la jeshi na kumwambia Paulo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mtoto wa kiume wa dada yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mtoto wa ndugu yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia juu ya shauri hilo baya, alikwenda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia juu ya shauri hilo baya, alikwenda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mtoto wa ndugu yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa umbu lake Paulo alipoisikia njama hiyo, akaja, akaingia bomani, akamjulisha Paulo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mupwa wa Paulo akapata habari ya vile watu wale wanavyovizia kumwua Paulo. Halafu akaenda katika upango wa waaskari na kumujulisha Paulo habari ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mjomba wake Paolo akasikia khabari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paolo khabari.