Acts 23:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi, akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana huyu kwako kwa maana ana jambo la kukuambia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo yule kiongozi wa askari akampeleka yule kijana kwa jemadari, akamwambia, “Paulo yule mfungwa aliniita na kuniomba nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukueleza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paulo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo ofisa wa jeshi akampeleka mpwaye Paulo kwa kamanda. Ofisa wa jeshi akasema, “Mfungwa Paulo ameniomba nimlete kijana huyu kwako. Ana kitu cha kukueleza.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi, akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana huyu kwako kwa maana ana jambo la kukwambia.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi, akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana huyu kwako kwa maana ana jambo la kukuambia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo yule mkuu wa maaskari akampeleka yule kijana kwa jemadari akamwambia, “Paulo, yule mfungwa aliniita na kuniomba nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukueleza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo yule kiongozi wa askari akampeleka yule kijana kwa jemadari, akamwambia, “Paulo yule mfungwa aliniita na kuniomba nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukueleza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paulo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi, akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana huyu kwako kwa maana ana jambo la kukuambia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule akamchukua akampeleka kwa mkuu wa kikosi, akasema: Mfungwa Paulo umeniita, akataka, nimpeleke kijana huyu kwako, yuko na neno la kukuambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paulo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mukubwa akaenda pamoja naye kwa jemadari na kumwambia: “Yule mufungwa Paulo aliniita, akaniomba nikuletee kijana huyu kwa sababu yuko na neno la kukuambia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paolo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia.