Acts 23:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye akasema, “Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule kijana akasema, “Wayahudi wamekubaliana wakuombe umpeleke Paulo kwenye Baraza la Wayahudi kesho kwa kisingizio kwamba wanataka kufanya uchunguzi wa kina kumhusu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kijana akasema, “Baadhi ya Wayahudi wameamua kukuomba umpeleke Paulo kwenye mkutano wa baraza lao kesho. Wanataka wewe udhani kuwa wamepanga kumwuliza Paulo maswali zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye akasema, “Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye akasema, “Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule kijana akasema, “Wayahudi wamekubaliana wakuombe umpeleke Paulo kwenye baraza lao kesho kwa kisingizio kwamba wanataka kufanya uchunguzi wa kina wa shauri lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule kijana akasema, “Wayahudi wamekubaliana wakuombe umpeleke Paulo kwenye baraza lao kesho kwa kisingizio kwamba wanataka kufanya uchunguzi wa kina wa shauri lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye akasema, “Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Wayuda wamepatana kukuomba wewe, umshushe Paulo kesho kwenye wakuu, kwamba wanataka kumwuliza kwa welekevu, mambo yake yalivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kijana akasema: “Wayuda wamepatana kukuomba umulete Paulo kesho katika Baraza Kubwa. Nao watakuambia tu kwamba wakubwa wa baraza wanataka kuchunguza vizuri zaidi maneno yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paolo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata khabari zake kwa usahihi zaidi. Bassi wewe usikubali;