Acts 23:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo nikaona kuwa alikuwa anashutumiwa kwa mambo yanayohusu sheria yao, lakini hakuwa ameshtakiwa kwa jambo lolote linalostahili kifo au kifungo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo nilivyoona: Wayahudi walisema mtu huyu alifanya mambo mabaya. Lakini mashitaka haya yalihusu sheria zao za Kiyahudi, na hakukuwa kosa lolote linaloweza kusababisha kufungwa au kifo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za Sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo nikaona kuwa alikuwa anashutumiwa kwa mambo yanayohusu sheria yao, lakini hakuwa ameshtakiwa kwa jambo lo lote linalostahili kifo au kifungo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo nikaona kuwa alikuwa anashutumiwa kwa mambo yanayohusu sheria yao, lakini hakuwa ameshtakiwa kwa jambo lolote linalostahili kifo au kifungo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaona, ya kuwa anasutiwa mashindano ya Maonyo yao, lakini hakuna neno linalompasa kuuawa na kufungwa tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikatambua kwamba wamemushitaki juu ya ubishi wenye kuelekea Sheria yao, lakini hakutenda kosa lolote linalomupasa kuuawa wala kufungwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sharia yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.