Acts 23:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumwua, niliamua kumleta kwako, nikawaambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na njama dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara moja. Niliwaagiza washtaki wake pia waeleze mashtaka yao dhidi yake mbele yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na vitimvi juu ya mtu huyu, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimeambiwa kuwa baadhi ya Wayahudi walikuwa wanafanya mpango wa kumwua. Hivyo nimeamua kumleta kwako. Pia nimewaambia Wayahudi hao wakwambie walichonacho dhidi yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumuua, niliamua kumleta kwako. Nikamwambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumwua, niliamua kumleta kwako, nikawaambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na shauri baya dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara, nikiwaagiza washtaki wake pia waeleze mbele yako mashtaka yao dhidi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na shauri baya dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara moja. Niliwaagiza washtaki wake pia waeleze mashtaka yao dhidi yake mbele yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na ghasia juu ya mtu huyu, mara nikamtuma kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumwua, niliamua kumleta kwako, nikawaambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena nilipoambiwa, ya kuwa mtu huyu anatunduiliwa, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza hata wenye kumsuta, waseme mbele yako, wanayomsuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na vitimvi juu ya mtu huyu, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati nilipopata habari kwamba Wayuda wanafanya shauri la kumwua, mara moja nikakusudia kumutuma kwako, nami nimewaagiza watu wanaomushitaki walete mashitaki yao kwako.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta nilipopewa khabari kwamba patakuwa na vitimbi juu ya mtu huyu, marra nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale walioshitaki, wanene khabari zake mbele yako. Salamu.