Acts 23:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
alisema, “Nitasikiliza kesi yako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya uliwali ya Herode.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Gavana akasema, “Nitakusikiliza Wayahudi wanaokushitaki watakapokuja hapa pia.” Kisha gavana akaamuru Paulo awekwe kwenye jumba la kifalme. (Jengo hili lilijengwa na Herode.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
alisema, “Nitasikiliza shauri lako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
alisema, “Nitasikiliza shauri lako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Nitakuuliza na kukusikiliza, wewe kukusuta watakapofika; kisha akaagiza, alindwe katika boma la Herode.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya uliwali ya Herode.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akamwambia: “Nitakusambisha wakati wale wanaokushitaki watakapofika.” Kisha akaamuru Paulo alindwe katika nyumba ya kifalme ya Herode.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nitakusikia maneno yako watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika praitorio ya Herode.