Acts 23:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa Torati ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lolote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wayahudi hawa wote wakaanza kubishana kwa kupaza sauti. Baadhi ya walimu wa sheria, waliokuwa Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hatuoni kosa lolote kwa mtu huyu. Inawezekana kwa hakika malaika au roho alizungumza naye.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kelele ziliongezeka na baadhi ya walimu wa Sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa sheria ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lo lote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa Torati ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lolote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wowote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakawa makelele makubwa; palikuwa na waandishi waliokuwa wa upande wa Mafariseo, wakainuka, wakabishana wakisema: Mtu huyu hatumwoni kiovu cho chote. Kama yuko roho au malaika aliyesema naye, hatutaki kumgombeza Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kukakuwa makelele mengi, na walimu wamoja wa Sheria waliokuwa wa chama cha Wafarisayo wakasimama na kubishana kwa nguvu, wakisema: “Hatuoni ubaya wowote juu ya mutu huyu. Labda roho au malaika wamesema naye!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Pakawa makelele mengi. Waandishi wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakamtetea, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema nae tusishindane na Mungu.